Wakulima kuwezeshwa na NCCR-Mageuzi

DAR-ES-SALAAM : CHAMA cha National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi) kimesema serikali yake itawezesha wakulima kupata zana bora za kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ya kisasa, kuboresha mifumo ya utoaji ruzuku na pembejeo.
Katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025–2030, chama hicho kimeeleza kuwa sekta ya kilimo imebakia nyuma kiteknolojia na katika uwezeshaji wa wananchi wanaoshiriki kwenye uzalishaji mali, huku wakulima wengi wakitegemea jembe la mkono na mvua.
“Tutawaunganisha wakulima na taasisi za fedha ili kukifanya kilimo kuwa cha kisasa na cha kibiashara chenye tija, ambapo mazao yake yataongezwa thamani kwa kuzalishwa bidhaa za kilimo na chakula kwa ajili ya soko la ndani na nje,” imeeleza ilani hiyo. SOMA: NCCR Mageuzi waipa tano serikali mkataba na Dp World
Aidha, chama hicho kimeeleza kuwa kitawezesha wananchi kujiendeleza kijasiriamali katika sekta ya kilimo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kuzalisha bidhaa za kilimo na mifugo pamoja na viwanda vya kusindika bidhaa tayari kwa matumizi ya binadamu na kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Ilani hiyo pia imeeleza kuwa wakulima wataelimishwa kuhusu kanuni bora za kilimo, miradi ya umwagiliaji, matumizi ya majosho, pamoja na kuongeza idadi ya maofisa ugani na washauri wa kilimo
“Tutatengeneza mpango imara na endelevu wa huduma za ugani katika kilimo na mifugo pamoja na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa mvua kwa kuongeza maeneo ya umwagiliaji,” imeeleza ilani hiyo. Vilevile, chama hicho kimebainisha kuwa kitafanya tathmini ya aina za mbegu bora zenye uwezo wa kutoa mavuno mengi, kustahimili mabadiliko ya tabianchi na zenye viinilishe, kwa kuboresha mfumo wa utafiti wa kilimo.
Matokeo ya tafiti hizo yatapanuliwa kwa wakulima kupitia vyuo vya kilimo na tafiti za mbinu bora za kilimo, ardhi, mbegu pamoja na udhibiti wa maradhi ya mimea na mifugo. Kwa upande mwingine, ilani hiyo imeeleza kuwa chama kitaimarisha ushirikiano na sekta binafsi na vyama vya ushirika kuanzisha viwanda vya kusindika mazao hususani kwenye maeneo ya uzalishaji sambamba na kuanzisha masoko yenye hadhi na mvuto wa kimataifa katika miji ya mipakani ili kuimarisha biashara na nchi jirani.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
I’m making over $25,000 a month working part-time. I kept hearing other people talk about how much money they were making online, so I decided to look into it. Well, it’s all true and has completely changed my life. This is what I do. Check it out by visiting the following link:
COPY THIS →→→→ http://Www.Cashprofit7.Site
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com