Wakulima Tabora wasifu ubora mbolea za TFC

TABORA; Wakulima wa Mkoa wa Tabora wameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluh Hassan kutokana na usimamizi wake madhubuti kuiwezesha Kampuni ya Mbolea ya Tanzania (TFC) kujikita katika usambazaji na kuuza mbolea za ruzuku kwa wingi na kuwafikia wakulima kwa wakati.

Mwenyekiti wa Chama cha Msingi Usindi kilichopo wilayani Kaliua, Joachim Herman, amesema awali mazao yao yalikuwa siyo bora kama sasa hivi kutokana na kuanza kutumia matumizi ya mbolea za aina ya NPK 12, 18 24 na CAN zinazosambazwa na TFC.

Amesema baada ya kuanza kutumia Mbolea za TFC, kilimo cha tumbaku kimekuwa na tija hususani ilipofikia kwenye uchomaji wa Tumbaku, ambapo awamu hii haikuoza na imekuwa nzito yenye rangi inayovutia sokoni.

Akizungumza TABORA; Wakulima wa Mkoa wa Tabora wameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluh Hassan kutokana na usimamizi wake madhubuti kuiwezesha Kampuni ya Mbolea ya Tanzania (TFC) kujikita katika usambazaji na kuuza mbolea za ruzuku kwa wingi na kuwafikia wakulima kwa wakati.

Mwenyekiti wa Chama cha Msingi Usindi kilichopo wilayani Kaliua, Joachim Herman, amesema awali mazao yao yalikuwa siyo bora kama sasa hivi kutokana na kuanza kutumia matumizi ya mbolea za aina ya NPK 12, 18 24 na CAN zinazosambazwa na TFC.

Amesema baada ya kuanza kutumia Mbolea za TFC, kilimo cha tumbaku kimekuwa na tija hususani ilipofikia kwenye uchomaji wa Tumbaku, ambapo awamu hii haikuoza na imekuwa nzito yenye rangi inayovutia sokoni.

Akizungumza na wakulima hao, Ofisa Kilimo Mwandamizi kutoka Bodi ya Tumbaku, Sosthenes Kikwelele, amesema katika soko wanapokea mitumba ya tumbaku 650 kwa siku kutoka Chama cha Msingi Usindi (AMCOS), ambapo mitumba hiyo imesibitishwa kuwa na viwango bora vinavyohitajika katika soko la dunia na kuwa na vigezo vinavyotakiwa.

“Tofauti na awali wakulima walikuwa na changamoto ya upatikanaji wa mbolea na kusababisha uchelewaji wa matumizi na kusababisha kuvuna tumbaku kidogo iliyo chini ya viwango, lakini tangu kuanza kutumia mbolea kutoka TFC, msimu huu wakulima wengi wamepata tumbaku ambayo imekidhi vigezo kwa madaraja tofauti,” amesema ofisa huyo.

Naye Daniel Mwakienda Mkulima wa mbogamboga na kabichi kutoka Kijiji cha Mabama, amesema awali alikuwa anatumia mbolea nyingi kwenye kupandia na alikuwa anapata mazao kidogo.

Baadhi ya maofisa wa TFC, wakiambatana na wanahabari walitembelea wakulima hao kwa ajili ya kutoa elimu ya matumizi bora ya mbelea, lakini pia kusikiliza ushuhuda kutoka kwa wakulima kuhusu kutumia mbolea zinazosambazwa na TFC.
-na wakulima hao, Ofisa Kilimo Mwandamizi kutoka Bodi ya Tumbaku, Sosthenes Kikwelele, amesema katika soko wanapokea mitumba ya tumbaku 650 kwa siku kutoka Chama cha Msingi Usindi (AMCOS), ambapo mitumba hiyo imesibitishwa kuwa na viwango bora vinavyohitajika katika soko la dunia na kuwa na vigezo vinavyotakiwa.

“Tofauti na awali wakulima walikuwa na changamoto ya upatikanaji wa mbolea na kusababisha uchelewaji wa matumizi na kusababisha kuvuna tumbaku kidogo iliyo chini ya viwango, lakini tangu kuanza kutumia mbolea kutoka TFC, msimu huu wakulima wengi wamepata tumbaku ambayo imekidhi vigezo kwa madaraja tofauti,” amesema ofisa huyo.

Naye Daniel Mwakienda Mkulima wa mbogamboga na kabichi kutoka Kijiji cha Mabama, amesema awali alikuwa anatumia mbolea nyingi kwenye kupandia na alikuwa anapata mazao kidogo.

Baadhi ya maofisa wa TFC, wakiambatana na wanahabari walitembelea wakulima hao kwa ajili ya kutoa elimu ya matumizi bora ya mbelea, lakini pia kusikiliza ushuhuda kutoka kwa wakulima kuhusu kutumia mbolea zinazosambazwa na TFC.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button