Wakusanya taarifa watakiwa kujisajili

TUME ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imetoa onyo la mwisho kwa taasisi zote zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi kujisajili kabla ya Aprili 8, 2026 ikibainisha kuwa hatua kali za kisheria zitaanza kuchukuliwa kuanzia Aprili 9 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Machi 26, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Emmanuel Lameck Mkilia amesema serikali imetoa muda wa kutosha tangu mwaka 2024 kwa taasisi kujisajili ikiwa ni pamoja na kuongeza muda huo mara mbili.
Amesema kuanzia Aprili 9, utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44 utaanza rasmi, na taasisi au mtu yeyote atakayebainika kutokujisajili atachukuliwa hatua za kisheria. SOMA: Epukeni ‘WiFi’ ya bure kulinda taarifa

Kwa mujibu wa sheria hiyo, adhabu kwa mtu binafsi ni faini ya kuanzia Sh 100,000 hadi Sh milioni 20 au kifungo cha hadi miaka 10 jela, huku taasisi na makampuni zikikabiliwa na faini ya kuanzia Sh milioni moja hadi kufikia Sh bilioni tano kulingana na uzito wa kosa.
Sheria hiyo inagusa sekta mbalimbali zikiwemo serikali, mabenki, hospitali, shule na kampuni za simu na inalenga kulinda faragha ya wananchi pamoja na kujenga imani katika huduma za kidijitali na kukuza uchumi wa kisasa.




Start making cash right now… Get more time with your family by doing jobs that only require for you to have a computer and an internet access and you can have that at your home. Starvt bringing up to $18012 a month. I’ve started this job and I’ve never been happier and now I am sharing it with you, so you can try it too. You can check it out here…
HERE→→→→→ https://PayAtHome1.Com/