Waliopanga uhalifu Bwawa la Nyerere wakamatwa Rufiji

Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji linawashikilia watuhumiwa sitini na 65 kwa makosa mbalimbali wakiwepo wahalifu walio kamatwa na vifaa vya mradi wa umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Akitoa taarifa hiyo leo Disember 7 2022 kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji kamishina msadiizi wa Polisi ACP Protas Mutayoba amebainisha kuwa Jeshi hilo liliendesha operesheni kali katika mkoa huo na kufanikiwa kukamata mtungi wa gesi uliokuwa unakwenda katika mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere.

Aidha kamanda Mutayoba amesema kuwa Jeshi hilo Pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wa madawa ya kulevya,pikipiki zinazotumika katika matukio ya uhalifu.

Katika tukio jingine Kamnda Mutayoba amesema Jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa mmoja kwa kosa la kukutwa na nyara za serkali na mitego ya kutegea wanyama hao. Ambapo amebainisha upelelezi utakapo kamilika jarada litapelekwa ofisi ya taifa ya Maisha kwa hatua zaidi.

Sambamba na hilo Mutayoba ameeleza kuwa Jeshi hilo liliendesha operesheni ya usalama Barabarani ambapo makosa elfu nne na thelathini na tano kwa makosa mbalimbali.

ACP Mutayo ametoa rahi kwa wananchi wote wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji kutoa taarifa za uhalifu na walifu kwa Jeshi hilo ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya walifu hao.

Habari Zifananazo

Back to top button