Walioua wawili kwa mawe kukiona!

MWANZA: JESHI la Polisi mkoani Mwanza limeanza msako wa kuwatafuta wahalifu waliojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu wawili kwa kuwashambulia kwa mawe na silaha za jadi wakiwatuhumu kuiba gunia moja la mpunga.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema Oktoba 31 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani  humo Wilbroad Mtafungwa amesema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 30 Mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni  katika Kijiji na Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi na kuwataja waliouawa kuwa ni Nkula Lameck (26) mkazi wa Mwamanga na Nzuri Kazungu (25) mkazi Inchobela wote wakiwa ni wakazi wa Magu.

Kamanda amesema wahalifu hao walijichukulia sheria mkononi wakiwatuhumu kuiba gunia moja la mpunga.

” Inadaiwa Nkula na mwenzake Nzuri Kazungu  walikuwa wamebeba mpunga kwenye pikipiki yenye namba za usajiri MC 989 CWU aina ya Kinglion iliyochomwa moto na kuteketea kabisa wakati wa tukio hilo wakitokea kijiji cha Budula-Ngudu wilayani Kwimba na walipofika Kijiji cha Mwaniko wilayani Misungwi ndipo walipozuiliwa na kuuawa na wahalifu hao waliojichukulia sheria mkononi…” amesema Kamanda Mtafungwa

Habari Zifananazo

Back to top button