“Wamiliki kumbi za starehe jisajilini mpate vibali”

DAR ES SALAAM: Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wamiliki wa kumbi za starehe kujisajili na kupata kibali cha kuendesha biashara kwa kufuata taratibu za kutoa huduma kwa usalama, ufanisi, na mbinu za kuongeza ubora wa huduma wanazotoa.

Katibu Mtendaji wa BASATA Dk Kedmon Mapana amesema kufanya usajili na BASATA kwa kumbi za starehe ni muhimu kwa sababu za msingi kuzingatia sheria na kanuni.

“Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa kumbi hizo zinafanya kazi kwa mujibu wa taratibu za usalama, afya, na burudani zilizowekwa na mamlaka husika.” Amesema Dk Mapan ana kuongeza

Advertisement

“kujenga aminifu kwa waateja usajili na BASATA kunaweza kujenga imani na uaminifu kati ya wamiliki wa kumbi za starehe na wateja wao. Wateja wanaweza kujisikia salama wanapojua kwamba kumbi wanazotembelea zimefuata taratibu zote za kisheria na zinaidhinishwa na mamlaka husika”Amesema Dk Mapana.