Wampongeza Rais Samia kutimiza miaka 65

Clouds TV kwa kupitia Kipindi chake cha Sentro Bash la Bimdash wameungana na watanzania wengine katika kusherehekea kumbukizi ya tarehe ya kuzaliwa kwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan aliyetimiza umri wa miaka 65 jana tarehe 27 Januari.

Uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kupitia kipindi hicho kinachokwenda hewani kila ifikapo saa moja na nusu jioni kila siku kilikua maalumu kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia.

Aidha wakati kipindi hicho kikiendelea kwenda hewani Viongozi mbalimbali wamepiga simu moja kwa moja studio na kutoa salamu zao za kumtakia kheri ya kuzaliwa Rais Samia.

Viongozi waliopiga simu na kuzungumza moja kwa moja ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Christina Mndeme amesema Rais Samia ni kiongozi shupavu na mwenye maono anamuombea kwa Mwenyeezi Mungu ampe uhai na hekima zaidi ili aendelee kuiongoza nchi ya Tanzani huku akiwataka watanzania kuendelea kumshkuru Mungu kwa kuwa na kiongozi msikivu.

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa taarab nchini pia ni Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki Khadija Kopa alitoa burudani na kuimba wimbo maalumu wenye mahadhi ya taarabu.

“Rais Samia mimi ni nduguangu namuombea mwenyeezi Mungu amzidishie nguvu na ari ya kuliongoza taifa na kumzidishia umahiri wake katika kulitumikia taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”amesema Khadija.

Kopa ameongeza kwa kusema kuwa Samia ameingia katika kipindi kigumu cha uongozi lakini hivi sasa kila Mtanzania anakula mema ya nchi katika nyanja mbalimbali kama wasanii ,wanamichezo amekuza michezo ikiwamo soka ambako amekua akitoa hamasa ya goli la mama, mchezo wa masumbwi” amesema Kopa.

Kopa ameongeza kwa kusema kuwa anamuombea kwa Mungu Rais Samia aendelee kuiongoza nchi kwa amani na kusema mama alipo wapo na huu ndiyo mwanzo wa ushindi.

Msanii mwingine ambaye ametumbuiza ni Barnaba Classic ambaye amesema anamshkuru sana Rais Mama Samia kwa sababu anawapenda sana wasanii huku akijinadi kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii ambao wanapata nafasi za kutoa burudani kwenye hafla nyingi za Serikali na hasa Ikulu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button