Wanafunzi 25 Chuo cha Mafunzo wapatiwa msamaha
ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amewapatia msamaha kwa kuwaachia huru jumla ya wanafunzi 25 wanaotumikia adhabu zao chuo cha Mafunzo.
Wanafunzi 15 wanatoka Unguja na wanafunzi 10 ni wa kisiwani Pemba.
Taarifa iiyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar inaeleeza kuwa ni kawaida kwa Rais wa Zanzibar kutoa msamaha kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Mafunzo katika maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar.



