Wanafunzi Mipango wajifunza fursa za kujiajiri

DODOMA: Wanafunzi kutoka Chuo cha Mipango ya Maendeleo ya Vijijini Dodoma walitembelea banda la Heifer International Tanzania katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane, ambapo walijifunza fursa za kujiajiri kupitia mnyororo wa thamani wa maziwa.

Katika banda hilo, walijadili mambo mbalimbali yaliyoibua mazungumzo muhimu kuhusu nafasi ya vijana katika kubadilisha kilimo cha Tanzania kupitia ubunifu, ujasiriamali na teknolojia.

Aidha, wanafunzi hao walionesha kuvutiwa na mbinu za Heifer, hasa msaada wa mafunzo, usaidizi wa kitaalamu na uunganishaji wa masoko.

Programu kama AYuTe Africa Challenge zilitajwa kama nyenzo muhimu zinazowasaidia vijana wabunifu kupata jukwaa, vifaa na uwekezaji wa kukuza suluhisho za kiteknolojia za kilimo, ili kuboresha mifumo ya chakula na kuchochea maendeleo jumuishi.

Heifer inaendelea kujitolea kuwawezesha vijana kuwa mawakala wa mabadiliko katika kujenga mustakabali endelevu na wenye usawa kwa sekta ya mifugo Tanzania.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button