Wanafunzi UAUTwapewa mafunzo akili mnemba

DAR ES SALAAM: Zaidi ya Wanafunzi 150 Kutoka Chuo cha United African University Of Tanzania (UAUT) kilichopo Dar es salaam wamepewa mafunzo maaalumu ya Akili Unde (AI) lengo likiwa ni kuendana na mabadiliko ya Tehama ya dunia ya sasa.
Prof Rwekaza Mukandala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema mafunzo hayo yaliyoanza Juni 9 ambayo yanatarajiwa kutamatika 20, 2025 amesema akili unde kwa sasa haikwepeki hivyo ina tija kwa taifa pindi ikitumika kwa namna bora ya itaongeza kasi ya maendeleo.

Mkandala amesema inavyoelekea kwa miaka ya mbeleni Akili Unde itakuja kutumika kwa elimu ya awali hivyo wananchi wawe nayo makini namna sahihi ya kuitumia.
Kwa upande wake Prof. Thierry Nouidui Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Cha United African University Of Tanzania (UAUT) amesema wameandaa mkutano huo kwasababu Akili Unde inatumika kwa sasa duniani na hakuna budi kukabilana nayo hivyo ni vyema kujua namna gani bora ya kuitumia katika dunia ya sasa.

Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho walioshiriki mafunzo hayo Vivian Kachweke na Colin Mark wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kwani asilimia kubwa kwa sasa watu wengi wanatumia akili unde na kwa wao inawarahisishia kwenye itendaji kazi wao.



