Wanafunzi wa kike Moro wanolewa ujasiriamali

MOROGORO: TAASISI ya  Kumbukumbu ya Celina Kombani iliyopo mkoani Morogoro imeazisha mradi  kufundisha ujasiliamali mdogo kwa wanafunzi wa kike unaolenga  kuongeza chachu ya kuwatoa watoto wa kike kuwa tegenezi kwa kuwajengea uwezo wa kujitafutia kipato ili kunufaika wao na kusaidia familia zao .

Mhasibu wa taaisis hiyo ,Joyce Mizambwa, amesema hayo katika shule ya Sekondadi Matombo , halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakati wa Mafunzo  ya stadi za ujuzi wa ujasiliamali yanayotolewa na Taasisi hiyo kwa wanafunzi wa kike wanaotarajia kuhitimu  masomo ya kidato  ha sita mwa huu (2026).

Mizambwa amesema  mrati huo ulianza kutekelezwa tangu mwaka jana (2025) kwa kuwafikia wanafunzi wa kike waliohitimu kidato cha nne katika halmashauri zote za mkoa wa Morogoro .

Amesema  mwaka huu wameanza na wanafunzi wa kidato cha sita wanaotarajia kuhitimu masomo yao mapema mwezi Mei 2026.

Mizambwa amesema Mradi huo ni endelevu na  unalenga kuwafiikia wanafunzi wa kike mkoa mzima, mpaka sasa wamewafikia  wanafunzi wa kike 414 katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro na Mvomero.

“ Mradi huu ni endelevu na tunatarajia baada ya kuwafikia wanafunzi wa kidato cha sita , awamu inayofuata  kuanzia Septemba ni kwa ajili ya wahitimu wa kidato cha nne” amesema Mizambwa.

Naye Mwanzilishi mwenza wa Taasisi hiyo,  Dorisia Edward amesema  mafunzo hayo yalihusisha  utengenezaji wa sabuni za maji na mafuta ya mgando ili wawezekujitafutia kipato pindi wanapohitimu masomo yao na kurejea majumbani au kwenda Vyuo Vikuu.

Hivyo amewataka wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato cha sita mwaka huu kubadilisha mitazamo yao na wazazi kuchukua hatua za kuwezesha vijana wao kujikwamua kiuchumi kupikia ujasiliamali mdogo .

“ Wanafunzi hawa wamepatiwa mafunzo ya utengenezaji wa sabuni za maji na mafuta ya mgando , hivyo wakipata usimamizi  na jamii inayowazuguka utawajengea ujasiri kwani bado wadogo ili waweze kuendelea” amesema Dorisia.

Dorisia amesema jitihada za kumkomboa mtoto wa kike zinapaswa kuanzia kwa wazazi wenyewe kubadilisha mitazamo kwa sababu baadhi wanaweza kusema hawana mitaji ya kuwapatia watoto wao.

“Wazazi  wanayonafasi ya kuwaunga watoto wao kwenye vikundi kuwapatia  mitaji midogo wakawasimamia vizuri itasaidia ,hata sisi tunaweza kuangalia namna ya kuwasaidia” amesema Dorisia.

Kwa Upande wake mwanafunzi wa kidato cha sita ,Zuhura Msuya aliyepata mafunzo ya ujasiliamali ameshukuru Taasisi hiyo kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamewapa mwanga mzuri wa kwenda kuanzia maisha pindi watakapo hitimu masomo yao.

Amesema kuwa hatua ya Taasisi hiyo kuwapatia mafunzo hayo bure  inatoa faraja kwao na kuahidi kwenda kufanyiwa kazi  ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kumkwamua  mwanamke kiuchumi.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo,  Mariam Madamba ameiomba Taasisi hiyo kutilia mkazo zaidi mafunzo hayo muhimu  kwa wanafunzi wa wanaohitimi kidato cha nne kwa sababu ndio ni miongoni mwa kundi kubwa linalokabiliwa na changamoto za kiuchumi kutokana na wengi wao kuishis mtaani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button