Wanafunzi waongezewa likizo hofu ya kipindupindu Zambia

WANAFUNZI wote nchini Zambia watachelewa kwa wiki tatu kurejea shuleni kutoka likizo kutokana na mlipuko wa kipindupindu.

Wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari walikusudiwa kurejea Jumatatu ijayo lakini sasa watarejea tena Januari 29, Wizara ya Elimu ilisema.

Wizara ya Afya ya Zambia ilisema visa 3,015 vya kipindupindu na vifo 98 vimerekodiwa tangu Oktoba 2023.

Hapo awali ilikuwa imeonya kwamba mlipuko huo unatishia “usalama wa afya” wa nchi.

Habari Zifananazo

Back to top button