Jengo la ghorofa laanguka kenya

BREAKING NEWS: Jengo la ghorofa lililokuwa likijengwa limeanguka katika Mtaa wa 9, eneo la Eastleigh jijini Nairobi, Kenya, huku kukiwa na hofu kwamba watu kadhaa huenda wamenasa kwenye vifusi.
Kwa mujibu wa taarifa za mitandao mbalimbali nchini humo, Idadi ya watu walioathirika na tukio hilo bado haijafahamika.
Mashuhuda wamesema kulitokea vurugu katika eneo la tukio, huku baadhi ya watu wakianza kupora mali.
Wamesema watu hao waliwarushia mawe wahudumu wa magari ya wagonjwa, hali iliyolazimisha magari hayo kugeuza njia kabla ya kufika eneo la tukio kuanza shughuli za uokoaji.



