Wanafunzi wapaza sauti katika tathmini ya elimu ya mwaka

WANAFUNZI kutoka shule za Msingi na Sekondari wameipongeza Serikali kwa ujenzi wa miundombinu bora na rafiki ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, ambayo imechagiza ufundishaji na ujifunzaji.
Hayo yamebainika leo Oktoba 24, 2025 jijini Dodoma, katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tathmini ya pamoja ya Sekta ya Elimu.

Mwanafunzi mwenye mahitaji maalum, kutoka Shule ya Msingi Dodoma, Mohammed Saidi, licha ya kupongeza juhudi zilizofikiwa amesisitiza kuzingatia mwenye mahitaji maalum, kwa kuwapatia vifaa vya kujifunzia kama vile vitabu, viti mwendo, walimu mahiri pamoja na kutambua vipaji walivyonavyo.
SOMA: Serikali yafanya tathmini ya elimu nchini
Wakichangia mjadala, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Viwandani, Nenelo Mdachi pamoja na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nzuguni, Zaituni Halfan, wamehimiza umuhimu wa kushughulikia changamoto za kimaadili zinazowakabili baadhi ya walimu.

Aidha, wamesisitiza kusimamia kikamilifu Mwongozo wa Adhafu ili kuimarisha nidhamu, maadili na maendeleo ya taaluma shuleni.
Naye Mohamod Idi kutoka Shule ya Sekondari Umonga ametoa rai ya kuongeza idadi ya walimu wa masomo ya Sayansi pamoja na kuelimisha wazazi na jamii kuhusu umuhimu wa mkondo wa Amali.
Lengo ni kuendelea kuwahamasisha wanafunzi kujiunga na mkondo huo ili kukuza maarifa ya vitendo na kuandaa wataalamu wa baadaye.




Freedom to work whenever I want — that’s what I love! I made $18,542 in a month doing this online. Check the details ———————⊃⫸ https://dailycash21.blogspot.com/