Wanajeshi watatu DRC watuhumiwa kwa mauaji

CONGO : SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International  limewatuhumu maafisa wakuu wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kuhusika na vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu.

Wanajeshi hao wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo kufuatia mauaji ya mwaka jana katika mji wa kaskazini mashariki wa Goma ambapo watu 56 waliuawa ni Constant Ndima Kongba ambaye  alikuwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini, Kanali Mike Mikombe Kalamba na Meja Peter Kabwe Ngandu.

Ripoti hiyo inasema kuwa wanajeshi hao walivamia hekalu la kikundi cha kidini huko Goma mnamo Agosti 30, 2023 na wengi  ni waathiriwa waliokuwa wanachama wa kundi la kidini ambalo kiongozi wake aliitisha maandamano ya kutaka mashirika ya kigeni yasiyo ya kiserikali na kikosi cha Umoja wa Mataifa kuondoka katika eneo hilo.

SOMA: DRC Congo na Rwanda kumaliza mapigano

Wakati huo, mamlaka zilisema kuwa watu 56 waliuawa, lakini ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa ambayo Amnesty ilipata nakala yake ilisema idadi ya vifo ilifikia watu 102, ikiwa ni pamoja na wanaume 90, wanawake wanane na wavulana wanne, huku wengine 80 wakijeruhiwa.

 

Habari Zifananazo

Back to top button