Wanakijiji wahimizwa ushirikiano na Polisi kuimarisha usalama

Wananchi wa Kijiji cha Minyaa mkoani Singida wamehimizwa kushikamana na kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi ili kuimarisha usalama katika maeneo yao.
Mkaguzi wa Polisi wa Kata ya Kinyeto, Insp Elizabeth Nashon ametoa wito huo huku akiwataka wananchi wasiwafiche wahalifu ndani ya familia bali wawafichue kwa ajili ya kulinda amani ya kijiji chao.
Insp Elizabeth amesisitiza kuwa jukumu la kumlinda mtoto dhidi ya ukatili si la mzazi peke yake bali ni la kila mwanajamii.
Ametoa wito kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa jirani yake, hasa watoto, ili kujenga jamii salama yenye mshikamano kwa maendeleo ya taifa zima.