DAR-ES-SALAAM: MWANAMITINDO Mstaafu wa kimataifa, Tausi Likokola ameishauri Tanzania itoe wanamitindo wengi bora wanaokidhi vigezo vya kimataifa.
Akizungumza na HabariLEO, Likokola ambaye pia ni mwandishi wa vitabu amesema mashindano ya urembo yalikuwa njia ya warembo kuingia kwenye fasheni bahati mbaya vigezo vinatofautiana.
“Ni muhimu msichana akiwa anaelekea kwenye fasheni, shule aendelee na wazazi wajihusishe kuhakikisha anakutana na watu sahihi wanaojua cha kufanya na kwenda na ‘portfolio’ yake,” amesema Likokola.
Akizungumzia uthubutu wa wasichana kwenye eneo hilo, Likokola amesema kipindi cha nyuma alipokuwa akifanya programu kwenye televisheni aligundua wasichana wengi wanahitaji kuingia kwenye fasheni ila kuna changamoto katika njia za kufanikisha hilo.
“Wote wanashirikana na kampuni kwa matangazo, maonesho, magazeti na wanalipana vizuri, ni kazi inayoheshimika na siyo kupoteza muda,” amesema Likokola.
SOMA: Wanamitindo watakiwa kuongeza ubunifu