Wananchi kuelimishwa taka kuwa fursa kiuchumi

DAR ES SALAAM: BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wadau wa mazingira, linatarajia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Taka “Taka Sifuri” kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya mbinu za kubadilisha taka kuwa malighafi au bidhaa nyingine, hatua inayolenga kuifanya taka kuwa fursa  kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 24, 2026, Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria wa NEMC, Hamadi Kissiwa, amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Machi 28 hadi Machi 30, 2026 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kaulimbiu ya kimataifa ni “Wezesha taka sifuri kwenye sekta ya chakula”, huku kaulimbiu ya kitaifa ikiwa ni “Taka ni Fursa”, na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Hamad Masauni.

Kissiwa amefafanua maadhimisho hayo yanalenga kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu taka, kwa kuhamasisha matumizi ya dhana ya 3Rs yaani Kupunguza (Reduce), Kutumia tena (Reuse) na Kurejeleza (Recycle) ili kuongeza ufanisi katika matumizi ya rasilimali na kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Amesema matumizi ya mbinu hizo itasaidia kupunguza kiwango cha taka kinachotupwa ovyo na kuchangia uzalishaji wa malighafi kwa ajili ya bidhaa nyingine, na hivyo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja na kwa Taifa.

Kissiwa amesema maadhimisho hayo pia yana lengo la kuangazia changamoto ya upotevu wa chakula duniani, ambapo takwimu zinaonesha kuwa utupaji wa chakula unachangia takribani asilimia 10 ya uzalishaji wa hewa chafuzi, hali inayochangia mabadiliko ya tabianchi na kuathiri ustawi wa jamii.

Aidha, amewakaribisha wananchi na wadau wa mazingira kushiriki katika maadhimisho hayo yatakayokuwa yakifanyika kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 11 jioni, yakijumuisha maonesho ya fursa za uwekezaji katika sekta ya usimamizi wa taka na ubunifu wa bidhaa zitokanazo na taka.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button