WANANCHI wa kijiji cha Chekereli Kata ya Mabilioni wilayani Same, mkoani Kilimanjaro wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama na kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Wakizungumza kijijini hapo mbele Mbunge wa Same Magharibi maarufu “Mwana wa Kaya”, David Mathayo akiwa katika ziara ya kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 aliyoipa jina la Operesheni Ahadi, Silvano Hussein na Leni Kivunge wamemuowomba mbunge huyo kwa kutatua changamoto hiyo ya muda mrefu ikiwemo kuangalia uwezekano wa kutoa rola za maji.
Kivunge amesema wanamshukuru mbunge Mathayo kwa kutoa mabomba ya maji 25 kwaajili ya kusaidia usambazaji wa maji hayo na kuondoa adha yawanawake kutembea umbali mrefu kusaka maji ya kunywa huku shughuli nyingine zikishindwa kuendelea.
“Tunaumwa matumbo na tunatumia maji ya mto ambayo si masafi sana kwa afya zetu lakini ujio wa mabomba haya utatutua ndoo kichwani sisi wanawake na watoto wetu kwa ujumla lakini tunashukuru umesikia kero yetu na umekuja na mabomba ya maji hapa,” amesema.
Naye mbunge wa jimbo hilo, Mathayo amesema amesikia kilio cha wanachi hao hivyo ametoa msaada wa mabomba 25 kwa ajili ya kusambaza kijijini hapo ili kuwasaidia kupunguza umbali wa kufuata maji.
“Sasa Chekereli ninawapatia rola za maji 25 kwa ajili ya kusambazia maji wananchi wangu wapate maji kwa sababu nao wamenipa kura mimi mbunge ili ikifika 2025 wakija hapa wakisema ntafanya hivi vile watakuta Mathayo keshafanya”
Mathayo amesema anajua kuwa wananchi wa eneo hilo walikuwa wakipata shida kubwa ya maji hivyo mradi huo utakapokamilika utasaidia kusambaza maji katika eneo la Chekereli ikowemo kinamama itasaidia kuwatua ndoo kichwani ili wasihangaike kwa sababu wamezaa mtoto wa kiume anaitwa Mathayo.