Wananchi Mtwara kumpokea Makamu wa Rais

MTWARA: WANANCHI mkoani Mtwara wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi anayetarajiwa kuwasili mkoani humo Novemba 11, 2026.

Akizungumza mkoani Mtwara leo Novemba 9, mwaka huu alipotoa taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Donald Msengi amesema Makamu huyo wa Rais anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo kuanzia Novemba 11 hadi 13, mwaka huu akitokea Mkoani Ruvuma.

Ziara hiyo ina lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya zote tano za mkoa huo pamoja na kuzungumza na wananchi.

“Makamu wa Rais anatarajiwa kuwasili mkoani mtwara Novemba 11, 2026 na ataanza ziara yake katika wilaya ya Nanyumbu Novemba 12, mwaka huu”amesema Msengi

amesema baada ya kutembelea wilaya ya Nanyumbu ataendelea na ziara yake katika Wilaya za Newala, Tandahimba na Mtwara ambako atapata fursa ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuongea na wananchi.

“Tunatarajia kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, mwaka huu Jumatano wilayani Masasi”

Aidha siku inayofuata Novemba 12, makamu huyo wa rais atatembelea Wilaya ya Nanyumbu na baada ya hapo ataendelea na ziara yake katika Wilaya za Newala, Tandahimba pamoja na Mtwara.

Amesema Novemba 13, mwaka huu Makamu huyo wa Rais atahitimisha ziara yake katika wilaya ya Mtwara na Masasi mkoani Mtwara kabla ya kuelekea mkoani Lindi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button