Wananchi Mtwara wahimizwa uchaguzi mitaa

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ameendelea kutoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa wale wote waliyojiandikisha na wenye sifa ya kupiga kura wasiache kutumia nafasi hiyo kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.

Akizungumza leo mkoani Mtwara alipotoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Mkuu huyo wa Mkoa amesema wananchi hao wajitokeze na kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo uchaguzi ili wakachague viongozi
kwa ajili ya maendeleo yao.

“Kutokana na umuhimu wa jambo hili, mheshimiwa Rais kwa nguvu yake ya kikatiba ametoa siku ya kesho (Novemba 27, 2024) kuwa ni siku ya mapumziko hivyo kwa umuhimu huo twende tukaonyeshe sisi nasi tujitokeze twende tukapige kura tukachague viongozi wetu kwa ajili ya maendeleo yetu, “amesema Sawala

Advertisement

Hata hivyo amewasihi wananchi hao kuwa baada ya kupiga kura warudi nyumbani wakapumzike kwa ajili ya kusuburi matokeo na wakishapokea matokeo hayo wawe watulivu kwani baada ya hapo maisha yaendelee kama kawaida baada ya kupata viongozi wao wataoshirikiana nao katika ujenzi wa taifa.

“Niendelee kuwaomba sana kupiga kura kwa amani na utulivu wetu, twende tukachague viongozi wetu kwasababu tunasema serikali za mitaa ni sauti ya wananchi tujitojeze kushiriki uchaguzi,”amesisutiza