Wananchi Mtwara watakiwa kuchangamkia fursa

WANANCHI mkoani Mtwara wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara hasa yanapotokea matamasha na shughuli zinazokusanya watu wengi.

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Mtwara Vijijini, Selemani Nampanye amezungumza hayo wakati wa kilele cha Tamasha la Nyangumi lililofanyika kwenye kata ya Msimbati Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Amesema kupitia matukio ya aina hiyo kuna fursa mbalimbali ambazo wananchi wanapaswa kuzichangamkia kwa kujiongezea kipato na kuwaomba kuendelea kulitangaza na kulipa uzito mkubwa tamasha hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kushiriki kikamilifu kwenye matamasha kama hayo ili waweze kutoa huduma ya elimu kwa mwananchi kupitia majukwaa hayo pia kudhamini ili tamasha hilo liweze kufanyika kwa ukubwa zaidi.

“Niwakalibishe taasisi zote za umma na binafsi zinazoweza kudhamini matamasha kama hayo ili yaweze kufanyika kwa ukubwa na ubora wa kitaifa na zilete tija zaidi ya kiuchumi kwa wananchi wetu,”

“Natamani nione tamasha hili mwakani linafanyika kwa ukubwa zaidi na kuwa na sura ya kitaifa, uchumi wa mtwara unategemea sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, uvuvi, mifugo na biashara ikiwa sasa sekta ya utalii nayo inakwenda kuwa tegemeo la kuongeza uchumi wa mtwara,” amesisitiza

Mmoja wa wananchi aliyeshuhudia tukio la nyangumi hao, Jamali Andenani amesema utalii huo ni mkubwa  kwa kutangaza mkoa ikizingatiwa nyangumi hapatikani kokote nchini tanzania huku akiipongeza serikali kwa jitihada kubwa inayofanya kwa kuendelea kusimamia kikamilifu masuala ya utalii.

“Hivi viumbe vipo duniani lakini pia vipo katika bahari yetu ya mtwara kwasababu wengi tunaamini tunapewa tu promosheni tu kuwa mtwara kuna nyangumi ila leo hii kupitia hii festival tume jionea wenyewe,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button