Wananchi Shinyanga waeleza changamoto za jamii

BAADHI ya Wananchi mkoani Shinyanga wameeleza changamoto zinazotokea kwenye jamii kukosa maadili, wizi na kutojituma kwenye kazi zinatoka na namna alivyolelewa.

Yuster James na Hamza Kusekwa wamesema hayo baada ya kusikiliza elimu ya sayansi ya makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto iliyotolewa na mtaalamu Andrew Nkunga kutoka Mtandao wa Malezi na Makuzi nchini (TECDEN).

Kusekwa amesema mtoto anatakiwa afundishwe tangu mimba inavyotungwa suala hili linapendeza lianze kufundishwa kwenye mikutano ya vijiji au vitongoji ili wananchi wapate kuelewa.

“Mimi mwenyewe nilikuwa sijui kama mama akiwa mjamzito mtoto tumboni anasikia kwenye hii ni sayansi ingekuwa hivyo basi hata vitendo vya mauaji,uhalifu visingekuwepo kumbe vinatokea wazazi chanzo kikubwa ”amesema Kusekwa.

Katibu wa Shujaa wa Maendeleo wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga, Daniel Kapaya amesema ameelewa vitendo vya ukatili vinaanzia wapi kumbe mtoto akiwa bado tumboni anasikia vitendo vinavyotokea viwe vizuri au vibaya kupitia programu hii kwa kujifunza wataendelea kutoa elimu kwa wazazi au walezi.

Mratibu kutoka kituo cha msaada wa sheria (paceshi) John Shija amesema kumekuwa na kesi nyingi za kutelekezwa watoto kutupwa na kukosa malezi ya wazazi ikiwa jamii nayo imesahau jukumu la malezi na hao wanaopewa kulea baadhi hawana nia juu ya malezi wanafuta pesa.

Mratibu mwandamizi wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga anayesimamia dawati la jinsia, Monica Venancy amesema programu jumuishi ya malezi na makuzi ameielewa namna ilivyo kumbe kizazi hiki kilichokosa maadili kuna sababu.

“ Kupitia program hii kwetu imekuwa ni msaada wazazi wangefuata utaratibu huo hata kulawitiana,kubakana na msongo wa mawazo kwenye jamii usingekuwepo zaidi kama ilivyosasa”alisema Venance.

Andrew Nkunga akitoa elimu hiyo amesema hatua za makuzi kwa mtoto zinaanzia umri 0 hadi miaka nane ikiwa ni kipindi ambacho mtoto ubongo unaanza kukua kama atapata changamoto kwenye ukuaji hata ukuaji wake hautakuwa timilifu.

Akitambulisha program ya PJT-MMMAM kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la Investing in Children and Strengthing their Society ( ICS ) Sabrina Majikata amesema Shirika la watoto Duniani (UNICEF ) na Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitengeneza nguzo tano kuhakikisha wanawekeza katika umri wa miaka mitatu lakini taifa la Tanzania liliangalia hilo nakuona kuwekeza katika umri wa mwaka 0 hadi minane.

Majikata amesema mtoto akiwa bado mdogo ubongo unahitaji kujijenga zaidi na kunatakiwa kutiliwe mkazo katika nguzo tano ambazo ni lishe,afyabora, malezi yenye mwitikio, ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale amesema taasisi zinazolea watoto ndani ya mkoa zinapatiwa mafunzo sababu zimekuwa zikiishi na watoto wenye umri mdogo kwa kusaidia wazazi wao ili wakue katika misingi bora.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amesema watoto wanatakiwa wakue katika utimilifu na kulelewa katika nguzo tano muhimu zilizotajwa.

“Tumeelezwa duniani kuna watoto taribani milioni 250 wenye umri chini ya miaka mitano na hapa Tanzania kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kuna watoto zaidi ya milioni 16 sawa na asilimia 27 hivyo tunapaswa kuwalinda ili wafikie hali ya ukuaji timilifu”alisema Mkude.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x