Wananchi Ugweno wapewa elimu ya fedha

Wajasiriamali pamoja na wakazi wa kata ya Ugweno, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro wameshiriki mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa katika Shule ya Sekondari Msangeni Kifula.
Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, yamewapa uelewa juu ya matumizi bora ya fedha, usimamizi wa bajeti, usajili wa vikundi vya kifedha, na umuhimu wa kuwa na akiba pamoja na bima kwa biashara na mali binafsi.
Kupitia filamu maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, washiriki wamejifunza kwa njia rahisi na ya kuvutia, lengo kuu likiwa ni kuwasaidia kudhibiti rasilimali zao za kifedha na kupunguza utegemezi.
Elimu hiyo ya fedha imebeba faida nyingi kwa wananchi hao mfano; kuboresha maisha binafsi, kuimarisha biashara ndogo ndogo, kuchochea maendeleo ya jamii na kukuza uchumi wa taifa.
Kwa pamoja, uelewa huo wa kifedha utawajengea wananchi misingi imara ya maisha endelevu, huku wakichangia katika ukuaji wa uchumi wa kitaifa kwa njia shirikishi na yenye tija.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button