Wananchi wapewa msaada wa kisheria Mtwara

OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na mawakili wa serikali wametoa msaada wa kisheria kwa wananchi mbalimbali mkoani Mtwara ili kuwasaidia katika matatizo mbalimbali yanayowakabili.

Akizungumza kwa niaba ya Wakili wa Serikali Mfawidhi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa ghafla fupi ya utoaji wa msaada huo wa kisheria kwa wananchi hao iliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, Neema Haule amesema wanawasikiliza wananchi kwa ajili ya kutatua kero zao mbalimbali ikiwemo mirathi,migogoro ya ardhi, talaka na mengine.

Amesema wananchi hao wanawasikiliza wote kwa pamoja na pale wanapoona kuna jambo linalohitaji ofisi nyingine kuliingilia kati huwa wanawaelekeza na zaidi wanawapatia mawasiliano ya ofisi zao zilizopo kwenye maeneo husika kwa ajili ya kuweza kuwapata mrejesho.

Hata hivyo kama watahitaji msaada zaidi wakaeleze hatua waliyofika ili waweze kufatilia kwa karibu yale masuala yao ambayo yamekuwa yakiwatatiza yaweze kufikia mwisho hivyo wanaendelea kuwakaribisha wananchi popote walipo kwa sasa hata ofisi zao zilipo wasisite kufika na kuendelea kupata kupata masaada huo.

‘’Tutaendelea kufanya haya kwa kila wakati hivi tumeanza lakini siyo mwisho tutaendelea kufanya kila mara kutoa msaada na kuwaeleza wananchi ofisi zetu zilipo ili kuendelea kupata msaada zaidi wa kisheria kwenye masuala yanayowatatiza kwenye jamii’’alisema Neema.

Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mtwara, Thimotheus Mophath amesema katika utoaji wa huduma hiyo wamekumbana na maswali mbalimbali hasa yaliyojikita katika mambo ya ardhi, miradhi pamoja na talaka hivyo wamejipanga kuisaidia jamii ili iweze kuondokana na matatizo hayo kwa kutoa elimu juu ya masuala hayo.

‘’Sisi mawakili ya serikali kwakweli tumegundua jamii yetu haina elimu ya kutosha juu ya masuala haya, wanaenda kugawana mali pasipokujua taratibu za kufata za kimahakama au wanaachana kiholela bila kujua kwamba kuachana katika mazingira ambayo mahakama haijuwi inakuwa haina nguvu kisheria’’ amesema Thimotheus

Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambaye pia ni mjumbe mwakilishi wa Chama cha mawakili wa serikali wa Tanzania kwa mkoa wa Mtwara, Justus Levocatus amesema huduma hiyo itakuwa ikitolewa mara tatu kwa mwaka lakini pia kutoa elimu kupitia vyombo mbalimbali ya habari ikiwemo redio ili waweze kuifikia jamii kwa ukubwa zaidi.

Baadhi ya wananchi waliyopatiwa huduma hiyo ya msaada wa kisheria na mawakili hao akiwemo Hussein Fundikila mkazi wa manispaa hiyo ‘’Tunawashukuru sana mawakili wa serikali kwa kuchukuwa jukumu hili la kuleta huduma hii moja kwa moja kwa wananchi bila gharama yoyote na kutusaidia katika masuala yetu mbalimbali tuliyonayo sisi wananchi kama vile miradhi na mengine’’

Mwananchi mwingine ni Magdalena Milanga mkazi wa manispaa hiyo, amesema amekuja kupata msaada huo juu ya mgogoro wa baina yake na mwajiri wake ambapo amezungumza na mawakili wamemuelekwa na kupatiwa ushauri wa kwenda kwenye ngazi za juu zaidi kupitia ofisi yake kuhusiana na tatizo lake hilo.

Hata hivyo zoezi hilo linaenda sambamba na kauli mbiu inayosema ’Uweledi na Ubora katika Utoaji Huduma ya Kisheria kwa Jamii’

Habari Zifananazo

Back to top button