Wananchi watahadharishwa athari za mvua Mtwara

WANANCHI mkoani Mtwara wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya uwepo wa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema wanafahamu yapo maeneo mengi mvua zinapozidi kunakuwa na mafuriko ikiwemo eneo la Kiyangu lililopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Hata hivyo baadhi ya maeneo mengine/kata mkoani humo ikiwemo Mahurungu, Halmashauri ya Mji Nanyamba katika Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara, lakini pia wilaya za Newala na Nanyumbu ambazo ziko chini ya Mto Ruvuma.

‘’Kwa wanaoishi maeneo hayo ni vema mkiona dalili hizo za mvua kubwa mkoandoka na kwenda maeneo ya juu kwa ajili ya usalama wenu vile vile ni vema katika kipindi hicho kuwa na tahadhari ya kuhifadhi chakula, kutumia mvua hizo vizuri katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.’’amesema Abbas

Hata katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka Krismasi na mwaka mpya 2024 ametoa tahadhari kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo ili kujiepesha na ajali zinazoweza kuzuilika.

Aidha amevielekeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama ngazi ya mkoa kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yote muhimu wakati wa kuelekea kwenye sikukuu hizo za mwisho wa mwaka.

‘’Ndugu wananchi wakati tukiendelea na maandilizi ya sikukuu naomba kutoa angalizo kwanza taadhari ya uwepo wa mvua nyingi kama ilivyokwisha kutolewa taarifa na mamlaka za hali ya hewa.’’amesema Abbas

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button