Kopa: Msiangalie mabaya ya wasanii tu

DAR ES SALAAM:MSANII nguli wa muziki wa taarabu nchini, Khadija Kopa, amewataka watengeneza maudhui na wanahabari wa mitandaoni kuacha kuangazia tu mabaya ya wasanii, badala yake wasaidie kuwashauri na kuwaelekeza mambo ya kufanya ili kuboresha maisha yao.
Akizungumza na HabariLEO, Kopa amesema watoa maudhui mitandaoni wanapaswa kujenga jamii, siyo kueneza tu taarifa hasi zinazohusu maisha ya watu maarufu.

“Wanaofanya umbea mitandaoni, wakizungumzia maisha ya watu, msiwaseme tu kwa mabaya. Elimisheni pia ni kitu gani sahihi wanachopaswa kufanya,” amesema na kuongeza kuwa habari mbaya kusambaa ni rahisi, lakini umuhimu unakuja pale ambapo mtoa taarifa anamwonesha mhusika njia sahihi ya kuboresha maisha yake.



