Wanawake 30 wanapoteza maisha kwa siku changamoto ya uzazi

MAKAMU wa Rais wa Chama cha Wakunga nchini, Loveluck Mwasha amesema kwa siku wamama 30 wanapoteza maisha kutokana na changamoto za uzazi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo hufanyika Mei 5 kila mwaka imewakutanisha wakunga na ya wadau mbalimbali kujadili changamoto na jinsi ya kuzitatua.

“Takwimu za vifo vya mama na mtoto bado vipo juu tunaongelea vifo 350 katika vifo laki Moja bado ipo juu ama vifo vya Wachanga kwenye 23 hadi 24 katika kila vizazi 1000 hivyo bado ni vifo vyingi,” amesema Mwasha.

Advertisement

Amefafanua kuna vifo 2030 ambvyo si vya lazima vinatokana na kumwagika damu nyingi wakati wa kujifungua au baada ya mda mfupi kujifungua na matatizo ya presha kuwa juu.

Mwasha amesema suala la mama na mtoto bado ni changamoto kubwa nchini na bado hawajafika kiwango kinacho kubalika.

“Ni zipi changamoto na nini kifanyike kama wadau kuondoa changamoto na kupunguza vifo vya mama na mtoto Moja wapo kuwapatia elimu bora wakunga,”amesema.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *