Wanawake GSM watoa msaada Segerea

DAR ES SALAAM :Wanawake wa Kampuni ya Gsm wametoa msaada kwenye gereza la mahabusu ya segerea ikiwa ni kutoa sehemu ya wanachokipata kwa kurudisha kwa jamii ikiwa leo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam, Faith Gugu Mkuu wa Gsm foundation wakati wakikabidhi msaada huo na kuongezea kuwa jamii inakumbushwa kuwakumbuka mahabusu hao kwani wana haki kama wengine .
Faith amesema misaada hiyo itasaidia kwa kiasi katika gereza hilo hivyo na jamii isiwatupe kwani wanastahili kusheherekea na haki sawa kama kawaida.
Kwa upande wake SSP Hamida Mussa Matimba Mkuu wa sehemu ya wanawake gereza la mahabusu segerea ameshukuru kwa msaada huo na kuisihi jamii kutokujihusisha na makosa yatakayoweza kusababisha kuwapeleka mahabusu.
Hamida ameongezea kwa kusema mtu kuwa magereza sio kwamba ni mkosaji bali kuna bahati mbaya imepelekea mtu kupelekwa hivyo jamii iwe makini na mambo maovu.
Kitaifa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake yanafanyikia leo mkoani Arusha na Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mgeni rasmi.



