Jengeni watoto wenye kuthamini amani

DIWANI wa Viti Maalumu Tarafa ya Suye mkoani Arusha, Michelle Mrema amewataka wanawake nchini kuendelea kuwa walezi wa amani, uvumilivu na mshikamano, akisisitiza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kuwalea watoto watakaokuja kuwa walinzi wa amani ya taifa.

Mrema ametoa rai hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru Wanawake wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani Arusha kwa kumuamini na kumchagua kuwatumikia. Hafla hiyo ilifanyika katika Kata ya Sokoni I, Jijini Arusha, ikiwa na kauli mbiu isemayo “Wanawake wa UWT ni msingi wa amani, uongozi na maendeleo ya taifa.”

Amesema ili taifa liendelee kubaki salama, wazazi na walezi wana wajibu wa kuwalea watoto katika misingi ya maadili, uzalendo na mshikamano, itakayowawezesha kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ya nchi. SOMA: MWONGOZO WA MALEZI: Msingi wa urithi wa familia bora

Katika hatua nyingine, amewasihi wazazi kuhakikisha watoto wote wanapata haki ya msingi ya elimu kwa kuwapeleka shule ifikapo Januari 2026, na kuahidi kuwa karibu na watoto yatima na wenye mazingira magumu, akisisitiza kuwa ni jukumu la jamii kushirikiana katika kuwalea na kuwawezesha kufikia ndoto zao.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I make up to $220 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $450h to $890h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now I am hoping I could help someone else out there by sharing this link.Try it, you won’t regret it!.

    HERE→→→→→→→→→→ https://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button