TANGA; Watu wanne wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali ya lori la mizigo (T 925 CAU) lililokuwa likitokea Wilaya ya Muheza kuelekea Tanga Mjini na kugonga gari aina ya Nissan Civilian (T 228 DPD) iliyokuwa imeharibika barabarani eneo la Tanganyika, wilayani Muheza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Maket Msangi amesema ajali hiyo ilitokea jana Juni 15, 2024, saa 3 usiku na kuwataja waliofariki ni Anwar Juma (30) ambaye ni kondakta, Shabi Omari (45) abiria, Hassan Abdallah (32) na mwanaume mmoja ambaye bado jina lake halijatambulika, anakadriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 25 na 30.
Majeruhi ni Juma Adam, Hussein Kombo, Mundhir Mwait na Sikujua Hamid, ambao hali zao ni nzuri na wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali Teule Muheza.