MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kwa Umoja wa Wajane Arusha juu ya mbinu za kuwaepusha watoto wao na tatizo la dawa za kulevya.
Wajane hao zaidi ya 250 wamefundishwa dalili za kutambua kama watoto wao wameshaanza kujihusisha na dawa za kulevya, pia wameelekezwa uhusiano uliopo kati ya dawa za kulevya na afya ya akili tukio lililofanyika Uwanja wa Sheik Amri Abeid Karume Arusha.
Elimu hiyo imetolewa na Mratibu wa Afya ya Akili Arusha, DC Pascal Kang’iria na Ofisa wa DCEA Kanda ya Kaskazini, Shabani Miraji ambapo amesisitiza wajane hao kutojiingiza katika makundi hayo badala yake wajikingea na viashiria vya matumizi ya dawa hizo
Umoja huo ulihamasishwa kushirikiana na mamlaka kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya katika maeneo yao kwa kupiga namba ya simu ya bure 119.