Wapinzani waguswa ahadi za Samia

VIONGOZI vya vyama vya upinzani wamesema Rais Samia Suluhu Hassan akitekeleza mambo aliyoahidi kuyafanya katika siku 100 tangu aapishwe, wananchi watapata manufaa makubwa.
Alitoa ahadi hizo wakati anazindua kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, Kawe mkoani Dar es Salaam, Agosti mwaka huu.
Samia aliapishwa Novemba 3 mwaka huu Chamwino mkoani Dodoma kuanza awamu ya pili ya kuiongoza Serikali ya Awamu ya Sita.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ally Khatib alisema Rais Samia akitekeleza ahadi hizo atajenga imani kwa wananchi kuhusu uongozi wake jambo litakaloimarisha mshikamano katika taifa na kupunguza hali ya kutofurahishwa na uongozi wa kisiasa.
“Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita watu waliona utekelezaji na utendaji wake na alifanya kazi kwa kasi kubwa ndio maana wamemchagua na sasa nina imani naye atatekeleza ahadi zake bila kuwaangusha wapigakura wake,” alisema Khatib.
Alisema akitekeleza ahadi zake ataimarisha uchumi wa taifa ukizingatia ahadi yake ya kuhamasisha uwekezaji na kukuza sekta ya kilimo na viwanda itachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi na kutoa ajira na itapunguza kiwango cha umaskini na kuhamasisha wajasiriamali wazawa.
Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Makini, Coster Kibonde alisema Rais Samia akitekeleza ahadi zake kwa ufanisi ndani ya siku 100 ataboresha huduma za kijamii ikiwemo, ahadi kuhusu kuboresha afya, elimu na miundombinu itachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya wananchi.
Kibonde alisema ahadi za kuboresha utawala bora, kupambana na rushwa zitaongeza uwazi katika utendaji wa serikali ufanisi na kuondoa matatizo yanayotokana na urasimu na ubadhirifu wa rasilimali.
Alisema huduma bora za afya na elimu zitasaidia kuondoa changamoto za afya na kujiandaa kwa mabadiliko ya kijamii, ambapo wananchi wengi wataweza kupata fursa nzuri za ajira na maendeleo.
Kibonde alishauri Samia atekeleze ahadi zake kwa weledi kwa sababu zilitokana na ilani ya uchaguzi ya CCM 2025-2030 ambayo ni mkataba kati yake na Watanzania.
“Kuna mambo mengine ambayo yanahitaji kipaumbele na hayakuahidiwa. Ninapendekeza licha ya kutekeleza ahadi hizo ahakikishe anaweka hali shwari ya taifa baada ya vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi kwa kuzungumza na makundi yote ili viongozi, vyombo vya usalama na wananchi waongee lugha moja,” alisema.
Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Kijamii (CCK), David Mwaijojele alisema Rais Samia akitekeleza ahadi zake ataimarisha maendeleo ya nchi na kurejesha umoja, utulivu na mshikamano.
Mwaijojele alimshauri Rais Samia aangalie vipaumbele yakiwemo mabadiliko ya katiba ya nchi.
“Asimamie maendeleo ya maisha ya watu, kuna baadhi ya Watanzania wanaishi maisha magumu sana aweke mbinu bora na zenye tija ambazo zitawatoa Watanzania kwenye hali ya umaskini hadi hali ya unafuu,” alisema.
Pia, Mwaijojele amemshauri Rais Samia aimarishe ushirikiano na sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine ili kuhakikisha rasilimali zinapatikana na zinatumiwa vizuri.
Alisema Serikali ya Rais Samia inapaswa kuwekeza katika miundombinu ya barabara, reli na bandari ili kuongeza ufanisi wa usafirishaji na kuunganisha maeneo mbalimbali ya nchi.
Aidha, alishauri Rais Samia kuzindua mpango wa kupunguza umaskini, kujenga mifumo bora ya usafiri husasani Mkoa wa Dar es Salaam, kuweka miundombinu bora ya utendaji kazi kwa watumishi wa serikali na sekta binafsi na kuvutia uwekezaji kwa ajili ya kuweka ubia katika uendeshaji wa baadhi ya huduma za jamii.
Katibu Mkuu wa Chama Tanzania Labour Party (TLP), Yustas Rwamugira alisema wakati anatekeleza ahadi hizo Rais Samia aimarishe ulinzi wa wananchi wake na nchi kwa mujibu wa katiba.
Rwamugira amemshauri kiongozi huyo awajenge vijana katika mazingira ya uwajibikaji kwa kuwapa nguvu ya kuwainua kiuchumi ili kuondoa umaskini na uhalifu unaoweza kufanywa kwa sababu ya ukosefu wa fedha na ajira.
Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Wakulima (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru alisema Rais Samia akitekeleza kwa wakati ahadi zake atarejesha matumaini ya wananchi.
“Dunia ya sasa imebadilika, watu wamekuwa na uelewa wapi wanapotoka na wanapokwenda, kila kinachofanyika wanakitazama kwa karibu sana, na wapo baadhi yao walikuwa wamepoteza matumaini na imani yao kwa wanasiasa kwa sababu walikuwa wanawaahidi lakini hawatekelezi,” alisema Mwiru.
Wakati anazindua kampeni zake, Samia alisema ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa kuwa Rais, serikali yake itafanya mambo 10 kwa manufaa ya Watanzania zikiwemo ajira 12,000 katika sekta za afya na elimu.
“Tutapiga marufuku hospitali kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa kwa sababu ya kudaiwa gharama za matibabu, tutakachofanya ni kuja na mfumo mwingine wa kuhakikisha jamaa wa marehemu wanalipa gharama lakini si kuzuia miili,” alisema.
Samia alisema kupitia Bima ya Afya kwa Wote serikali itazindua mfumo wa taifa kwa awamu ya majaribio kuanzia kwa wazee, wototo na wajawazito.
“Gharama za matibabu zitabebwa kupitia mfuko wa bima ya afya. Pia, serikali itagharamia kwa asilimia 100 wananchi wasiokuwa na uwezo kupata vipimo vya figo, moyo, sukari, mishipa ya fahamu na mifupa,” alisema.
Samia alisema ndani ya siku 100 serikali yake itatoa ajira 5,000 katika sekta ya afya wakiwemo wauguzi na wakunga ili kuimarisha utoaji wa huduma ya afya ya mama na mtoto.
Alisema pia muda huo serikali yake itaweka mkakati wa elimu kisayansi ambao kila mtoto wa darasa la tatu awe na uwezo wa kusoma, kuhesabu na kuandika bila shida na itaajiri walimu 7,000 wa masomo ya hisabati na sayansi.
“Pia tutazindua mpango wa pamoja utakaohusisha waajiri, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu kulinganisha mafunzo na mahitaji ya sekta za kipaumbele, lengo ni kuwafanya wanafunzi wa VETA kuchukuliwa viwandani kufanya kazi za mazoezi kwa vitendo,” alisema Samia.
Alisema pia serikali yake itatenga Sh bilioni 200 za kuwezesha upatikanaji mitaji kwa wafanyabiashara wadogo na kati, uanzishwaji kampuni changa, kurasimisha wajasiriamali wadogo wakiwemo bodaboda, mamalishe, wafanyabiashara wadogo kuingizwa katika mfumo rasmi wa serikali.
Samia alisema serikali itaanzisha programu ya mitaa ya viwanda wilayani kwa lengo la kuzalisha ajira kupitia mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, madini na misitu.
Pia, alisema katika kipindi hicho serikali itakayoiunda itaanza ujenzi wa gridi ya taifa ya maji ili kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji ambayo pia itahusisha vyanzo vikuu vya maji ambavyo ni Ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa na mito mikubwa.
Samia ameahidi kuendeleza jitihada za nishati safi kupikia kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, kuweka mifumo rafiki ya uwajibikaji kwa mawaziri na wakuu wa mikoa kutakiwa kutoa taarifa na kujibu maswali kwa wananchi kwa njia ya simu.
Alisema serikali itaendelea na mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia na sekta binafsi ikiwemo kuunda tume maalumu ya kuandaa mazingira ya mchakato wa katiba mpya.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………. http://www.job40.media