Wasanii washindwe wenyewe tu!
DAR ES SALAAM: Filamu zaidi ya 120 za wasanii wa Tanzania zimenunuliwa na chanel mpya ya St Swahili Plus chini ya Startimes Media kwa ajili ya kuoneshwa kwa watazamaji.
Akizungumza Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa chanel hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa amesema hiyo yote ni kuunga mkono juhudi za wasanii katika kazi zao lakini pia, kuhakikisha wanatoa burudani kwa Watanzania.
“Tumeanisha chanel ambayo asilimia 60 ya maudhui yanatoka ndani ya nchi. Tumetoa fursa kwa wasanii kwa kununua kazi zao ili na wao waweze kunufaika lakini pia na watazamaji wetu waburudike” alisema.
Malisa amesema uzinduzi huo umeenda sambamba maudhui mengine ya chaneli nyingine mpya kama ST Toons, ST Toonie, ST Kids Plus, ST movies kwa ajili ya kuonesha vipindi mbalimbali vya tamthili, watoto na filamu.
Mwakilishi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) Edward Nnko aliwapongeza Startimes kwa kutoa fursa kwa Watanzania akisema imekuwa ikitoa nafasi ya watu mbalimbali duniani kujifunza Kiswahili kupitia vipindi tofauti
Mwakilishi wa wasanii Rashid Mrutu amesema tangu Mwaka 2018 wamekuwa wakikusanya maudhui mbalimbali ya filamu na wamehusika kukusanya filamu nyingi za Kitanzania.