Washindi shindano la mavazi kuwakilisha vazi la taifa

SEIKALI imeliambia Bunge kuwa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu upatikanaji wa Vazi la Taifa inatarajia kuwashindanisha wabunifu wa mavazi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ili watakaokuwa washindi kwa upande wa wanaume na wanawake mavazi yao yapendekezwe kuwa vazi la Taifa.

Kauli hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma leo Februari 7, 2024 na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri, Dk Damas Ndumbaro lililoulizwa na mbunge wa Malinyi,  Antipas Zeno Mgungusi aliyetaka kujua maendeleo ya mchakato wa kuwa na Vazi la Taifa.

Waziri Mwinjuma ameongeza kuwa wabunifu hao watafanya kazi kwa kutumia maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wadau pamoja na wananchi ili kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa Vazi la Taifa kwa ufanisi na haraka zaidi akiwahakikishia Wabunge kuwa vazi la Taifa litapatikana ndani ya mwaka huu.

Advertisement