Washindi wa gofu wapewa tuzo Dar

DAR ES SALAAM: VIPAJI vya mchezo wa gofu vimeendelea kuthaminiwa kwa makundi mbalimbali ya vijana wa kike na kiume baada ya Kampuni ya Simu ya Vodacom kutoa tuzo kwa washindi wa mashindano ya Vodacom Corporate Masters.
Tuzo hizo zimetolewa kupitia kitengo cha Vodacom Business kinachoshughulika wafanyabiashara wakubwa pamoja na wadau mbalimbali wa michezo. Hafla hiyo imefanyika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam.
Aidha, mashindano yaliyolenga kuhamasisha ushiriki wa wadau kutoka sekta mbalimbali kupitia michezo ya kijamii ikiwemo.
Kampuni hiyo imeendelea na dhamira yake ya kuunga mkono michezo, kukuza vipaji na kudumisha uhusiano wa kijamii na wadau wake wa karibu.