WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Haorun Ali Suleiman, amezishauri nchi za Bara la Afrika, kutoa kipaumbele kwa mameneja na wasimamizi rasimaliwatu, kujiendeleza kitaaluma ili kuongeza ufanisi wa kila siku wa watumishi wa umma katika nchi zao.
Sulemain ametoa ushauri huo jijini Arusha wakati akifunga mkutano wa tisa wa Mtandao wa Mameneja na Wasimamizi wa Rasilimali Watu, katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet), wenye kauli mbiu “Uhimilivu wa Utawala na Ubunifu Kukuza Sekta ya Umma yenye Uelekeo wa Baadae Kupitia Uongozi wa Rasilimaliwatu.
“Ni wakati muafaka sasa kwa nchi zetu za Afrika kuhakikisha kuwa mameneja na wasiamizi rasilimaliwatu kujiendeleza, ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia watumishi wa umma, ili kuongeza ari katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi wetu,”amesema.
Naye Katibu Mkuu kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Zena Ahmed Said amesema kuna nchi ambazo zimefanya vizuri ikiwemo nchi ya Tanzania katika sekta ya utumishi wa umma ambapo imepata tuzo ya kimataifa hivyo ni vema nchi nyingine zikajifunza kutoka nchi zilizofanikiwa.
Wakati huo huo ,Rais wa APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi wa umma na Utawala Bora, Xavier Daudi amesema mkutano huo, umekuwa na manufaa makubwa ambapo washiriki wamebanidilishana uzoefu pamoja na kuweka maazimio ambayo yatatekelezwa na kila nchi ili kuongeza ufanisi katika sekta hiyo.
APS-HRMNet unaundwa na wanachama kutoka Bara lote la Afrika ambao wamegawanyika katika Kanda tano ikiwemo Afrika Magharibi yenye nchi 17, Afrika Mashariki nchi 10, afrika ya kati nchi 8, Afrika Kaskazini nchi 6 na nchi za Kusini mwa Afrika 13 ambapo Mawaziri wenye dhamana ya utumishi wa umma, makatibu wakuu,na wataalam mbalimbali kutoka barani Afrika.