Wasio na vigezo kupata nafuu mikopo Kigoma

KIGOMA: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Kigoma, Jamal Tamim amesema yupo tayari kuweka mali zake dhamana ili halmashauri za Kigoma zitoe mikopo ya halmashauri kwa vikundi visivyokuwa na vigezo.

Tamim amesema hayo leo Februari 3, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko la kwa Noti Ujiji mjini Kigoma wakati wa uzinduzi maadhimisho ya kimkoa ya miaka 49 ya kuzaliwa CCM.

Mwenyekiti huyo amesema uwepo wa idadi kubwa ya wasichana, vijana na watu wa makundi maalumu ambao wana shughuli za kiuchumi na shughuli zao zinafanyika kwa tija jambo hilo lina mchango mkubwa wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini kwa wananchi wa kipato cha chini.

Awali, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid amesema ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Revocatus Chipando (Baba Levo) ya kuboresha mazingira na miundombinu ya hilo iko pale pale na kwamba maboresha ya ramani yamesbabisha kuchelewa kidogo kwa ahadi hiyo na kwamba ramani hiyo ikikamilika mpango utaanza kutekelezwa.

Akizungumzia kuhusu mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri Maulid amesema kuwa halmashauri hiyo tayari imeshatoa kiasi cha Sh milioni 600 kwa vikundi 66 vya wajasiliamali na kwamba mkazo umewekwa kwa vikundi zaidi kupewa mikopo hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button