Wasioendeleza machimbo Makaa ya Mawe kufutiwa vibali

WAZIRI wa Madini Dkt Dotto Biteko ametoa miezi mitatu kwa Tume ya Madini kufanya uchambuzi wa kina na kubaini waliohodhi maeneo makubwa ya uchimbaji wa makaa ya mawe bila  kuyaendeleza  wafutiwe vibali na kupatiwa kwa wawekezaji wengine.

Biteko ametoa maagizo hayo leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa Madini ya makaa ya mawe ambao unafanyika leo November 15 Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

“Naelekeza Tume ya Madini baada ya muda wa miezi mitatu kuanzia sasa wafute lesseni hizo  kkwa mujibu wa sheria ya Madini Sura 123 ,” amesema.

Waziri ametoa maagizo hayo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kusema kuwa zipo baadhi ya kampuni na watu binafsi waliohodhi maeneo yao bila kuyaendeleza huku akiomba wizara ya Madini kuangalia suala hilo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x