Wasiozingatia mipaka uchimbaji madini kukiona

NAIBU Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa ameufungua mgodi wa dhahabu unaomilikiwa na mwekezaji mzawa, Godfrey Bitesigirwe uliopo kijiji cha Kilimamzinga kata ya Kang’ata wilayani Handeni mkoani Tanga na kuwataka wachimbaji wote kuheshimu mipaka ya leseni ya mwenye mgodi vinginevyo watachukuliwa hatua.

Mbali ya hilo pia waziri Kiruswa ametoa onyo kwa wachimbaji wadogo kuacha mara moja tabia ya kutorosha madini hayo kwa njia ya panya bila kulipa ushuru wa serikali na kusema kuwa serikali haitawaacha salama pindi watakapokamatwa.

Dk Kiruswa alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kilimamzinga mara baada ya kutembelea mgodi huo na kupata maelezo kwa mwekezaji mzawa anayemiliki leseni nane za uchimbaji dhahabu na kusikiliza kero za wachimbaji wadogo, mwekezaji mzawa na viongozi wa kijiji na kata.

Kiruswa alitoa maagizo kwa wafanyabiashara wasio na leseni kushirikiana na mwekezaji katika shughuli za uchimbaji pia alimwagiza mwekezaji poto{mdomo wa kuingilia mgodini ili kuondoa changamoto ya kuwa na mashimbo mengi yenye kuharibifu wa mazingira na kuepusha mianya ya utororoshaji.

Dk Kiruswa alitoa onyo kwa askari polisi waliopewa dhamana ya ulinzi eneo hilo kushiriki utoroshaji wa madini kuacha mara moja tabia hiyo kwani inajenga sifa mbaya kwa jeshi hilo.

Alisema na kuwataka wachimbaji wadogo kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo kwa siku 90 kwa kufuata leseni zao zinavyowaelekeza na anayeshimu maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando ya awali ya kuufunga mgodi huo.

Akizungumzia utoroshaji wa madini ya dhahabu, Dk Kiruswa ametoa anyo kwa wachimbaji wadogo na wafanyabishara wa madini wanaotorosha madini kwa lengo la kukwepa kodi ambapo amewataka kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na serikali ikiwemo kuuza madini katika masoko na vituo vya ununuzi wa madini vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Waziri Kiruswa alitoa muda wa mwezi mmoja kuondoa vibanda vyote vilivyoko katika mgodi huo na kufukia mashimbo ambayo hayatumiki na kuwataka wachimba kupanda miti ili kulinda mazingira.

Alisema serikali itamlinda mwekezaji mwenye kutambulika na serikali kwa gharama zote kwa kuwa analipa kodi ya serikali na serikali itawalinda wachimbaji wadogo wadogo watalindwa na serikali kwa huruma kwa kuwa ni wavamizi katika mgodi huo.

‘’Serikali haina msalimia mtume kwa watoroshaji wa madini ya aina yoyote hivyo basi kwa wale wenye nia ovu dhidi ya madini ya dhahabu kwa kutaka kujitajirisha haraka haraka na kukwepa kodi ya serikali rungu halitawacha salama’’

‘’Serikali itamlinda mwekezaji wa gharama yoyote kwa kuwa inamtambua kwani ndio tuliompa leseni na kingine analipa kodi kubwa ya serikali’’alisema Kiruswa

Naye Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini, John Sallu amempongeza Dk Kiruswa kwa kuumaliza mgogoro uliokuwepo katika eneo hilo ili wachimbaji wadogo wa dhahabu waweze kunufaika na rasilimali hiyo iliyopo katika kijiji hicho na serikali ngazi zote ziiweze kunufaika na kodi.

Sallu ameiomba Wizara ya Madini kutenga maeneo  kwa ajili ya wachimbaji wadogo hususan maeneo yenye leseni ya utafiti yaliyoisha muda wake ili waweze kufaidika na rasilimali madini zilizopo wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya mgodi kufunguliwa ,Bisitegirwe kwanza aliishukuru serikali kwa kufunguliwa mgodi wake na kuahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya mgodi kwa kuweka mdomo mmoja wa kuingilia ndani ya mgodi.

Mwekezaji huyo ambaye kwa sasa ameajiri wafanyakazi zaidi ya 94 ameahidi kutoa ajira kutoana na uzalishaji na kuahidi kuwa na mahusiano mazuri kwa jamii ikiwa ni pamoja na kutoa miaasa pindi anapohitajika kwa faida ya wakazi wa kijiji kufaidi rasilimali ya madini ya dhahabu.

Alisema atahakikisha anathibiti utoroshaji wa madini ya dhahabu kwa wachimbaji wasiokuwa na leseni wanofanya uchimbaji haramu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Alan Campbell
Alan Campbell
3 months ago

Im making over $28k a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they can make online so I decided to look into it. Well, p it was all true and has totally changed my life. This is what I do.
AND GOOD LUCK.:)
HERE====)>   https://www.salarybiz.com

Last edited 3 months ago by Alan Campbell
Kim
Kim
3 months ago

Last month i managed to pull my first five figure paycheck ever!!! I’ve been working for this company online for 2 years now and i never been happier… They are paying me $95/per hour and the best thing is cause i am not that tech-savy, they only asked for basic understanding of internet and basic typing skill… It’s been an amazing experience working with them and i wanted to share this with you, because they are looking for new people to join their team now and i highly recommend to everyone to apply… 

Visit following page for more information………..>>>  http://www.Richcash1.com

Last edited 3 months ago by Kim
Mining Census 2023
Mining Census 2023
2 months ago

Mining Census 2023

Watanzania mnakaribishwa kwenye SENSA ya Madini 2023 yenye lengo la kujua idadi ya migodi Tanzania, Idadi ya wachimbaji au watanzania wanaoshughulika na sekta ya Madini, Hali ya uchimbaji wa madini (zana zitumikazo kwa kila mgodi) na mapendekezo ya mbinu za kuboresha Sekta ya Madini.

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x