Watafiti wapendekeza huduma za maji na umeme bure

IRINGA:Utafiti uliofanyika mwaka 2022 na wataalamu wa Quanah Schools kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali nchini, umebaini kuwa huduma za maji na umeme bure zinaweza kutekelezwa nchini Tanzania bila kuathiri ustawi wa uchumi wa taifa, endapo serikali itaweka mfumo mahsusi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, mmoja wa watafiti hao, Mesia Lufingo, alisema, utafiti huo ulilenga kutathmini haki ya wananchi kupata huduma za msingi za kijamii kama maji na umeme bila vikwazo vya kiuchumi.
“Kila mtu ana haki ya kupata maji na umeme. Katika tafiti zetu tunatambua haki hiyo, kwahiyo si sahihi mtu kukosa huduma hizo kwa sababu hana pesa,” alisema Lufingo.
Mapendekezo ya wataalamu hao yameainisha kuwa, kila kaya inapendekezwa kupata maji bure kwa matumizi ya kunywa pekee, ambapo watoto wanapendekezwa kupata nusu lita kwa siku, wazee lita moja, na vijana kati ya lita moja na nusu hadi mbili.
Aidha, kwa upande wa nishati, wataalamu wanapendekeza umeme wa bure wa taa mbili kwa kila kaya—moja ya nje na moja ya ndani—ili kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa mwanga wa kusomea nyumbani.
“Tunataka huduma hizi ziwe bure, siyo tu bei nafuu. Gharama tulizokadiria kwa kaya moja kwa mwaka ni Sh1,538 kwa maji na Sh8,290 kwa umeme. Hii ni gharama ndogo ukilinganisha na athari za kukosa huduma hizi,” alisema Lufingo.
Kwa mujibu wa makadirio hayo, endapo mpango huo utatekelezwa kwa Watanzania wote, serikali itabeba mzigo wa takriban Sh bilioni 141.1 kwa mwaka, kiasi ambacho wataalamu wanakiona kuwa ni kidogo ukilinganisha na bajeti ya taifa na faida ya kijamii itakayopatikana.
Wataalamu hao wameeleza kuwa pendekezo hilo linajengwa juu ya uzoefu wa Afrika Kusini, ambako tangu mwaka 2001 serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa Free Basic Services (FBS), unaotoa huduma za maji na umeme bure kwa kaya maskini.
Katika mpango huo, kila kaya hupatiwa lita 6,000 za maji kwa mwezi bure, na uniti 50 za umeme bila malipo, hali iliyosaidia kupunguza umaskini wa nishati (energy poverty) na magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi.
“Mfumo wa Afrika Kusini umeonyesha mafanikio makubwa katika kuboresha afya, elimu na usawa wa kijamii. Hata Tanzania inaweza kujifunza, kwa kubuni mfumo wa kugharamia huduma hizo kupitia kodi za kifahari, ruzuku za nishati, au mapato yasiyo ya moja kwa moja,” alifafanua Lufingo.
Wataalamu wanasema wakati huu vyama vya siasa vikiendelea kushindana kutafuta ridhaa ya wananchi kuelekea uchaguzi, kujadili sera za kijamii kama hii ya huduma bure ni muhimu.
“Tunakaribisha wadau wote waungane nasi kuboresha mapendekezo haya. Lengo letu ni Tanzania yenye usawa wa kijamii,” alisema Lufingo.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com