Watafiti watakiwa kuachia matokeo ya tafiti zao

WATAFITI wametakiwa kutoa matokeo ya tafiti zao ili ziwanufaishe wananchi katika kuhakikikisha  changamoto za jamii zinatatuliwa sambamba na kukuza uchumi.

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko wakati akifingua Kongamano la 3 la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Ukuaji wa Uchumi lilioandaliwa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).

Advertisement

Amesema katika ushindani wa uchumi utafiti ndio unaweza kuleta maendeleo kwa kutumia tafiti zinazofanywa na watafiti wa ndani katika sekta mbalimbali na kutoa matokeo chanya yanayokana na tafiti atamizi zinazotatua changomoto za wananchi na si kubaki katika makabrasha pekee.

Amesisitiza kuwekeza zaidi tafiti zenye tija ili kutoa matokeo ya changamoto zilizopo kwa kutoa matokeo ya tafiti zinazofanywa kwa wananchi hivyo alitoa rai kwa watanzania kuamka na kuamua kwa uhalisia katika kutatua changamoto zinazokabili jamii haswa katika uhalisia wa jambo fulani.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na  Biashara, Exaud Kigahe kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema ni wakati muafaka wa tafiti zinazotolewa na wataalamu hao kuanzia kuzitumia kwa wananchi ili kuleta tija katika maendeleo sanjari na kudadavua kwa kina juu ya mwelekeo wa uchumi haswa katika ubunifu wa biashara na uchumi hususan katika tafiti atamizi

Huku Mwenyekiti wa Bodi ya  Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA), Profesa Jehovaness Aikael  amesema mtaji na ubora wa rasilimali watu ni nyenzo muhimu katika kuhakikikisha ukuaji wa uchumi ikiwemo mchakato wa kuongeza pato halisi la taifa na la mtu mmoja mmoja ikiwemo ongezeko la uwezo wa uchumi katika kuzalisha bidhaa na mabadiliko ya ubora wa watu.

” Watafiti lazima kuendelea kufanya tafiti zaidi katika uwekezaji, usimamizi wa biashara ndani na nje ya nchi ili kuiamrisha uchumi ikiwemo ushauri elekezi kwa wanataaluma na kuhakikikisha zaidi ubunifu,ugunduzi na uwekezaji katika kuhakikikisha nchi inakua zaidi kiuchumi ikiwemo uboreshaji mazingira ya biashara na kufikia malengo ya milenia,” amesema.