Watakiwa kuchangamkia fursa Nanenane Dodoma

DAR ES SALAAM; WADAU mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi, wametakiwa kuchangamkia fursa ya kupata sehemu za maonesho katika maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kuanza Agosti 1 hadi 8 ,2025 jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Ushirika Village,Ally Nchahaga ameeleza kuwa maeneo hayo maalum yanapatikana kwenye viwanja vya Nanenane ambayo yatakuwa na mabanda zaidi ya 100.
“Tumeandaa mahususi kwa wadau wa mendele kama madini, kilimo, biashara walete bidhaa zao na vitu wanavyofanya walete hapa katika viwanja vya Nanenane,” amesema Nchahanga.
Ameongeza; “Tutakuwa na vibanda zaidi ya 100 itawawezesha kuonekana na wananchi mbalimbali wataokuja kutembelea mabanda hayo ni ya kipekee, ambayo wana ushirika tumekuja nayo ili kuvutia wananchi kuonesha bidhaa mbalimbali kwa mpangilio katika ushirika Village.”
Nchahanga amesema wadau wanaoweza kushiriki katika maeneo hayo maalumu kama vile mashirika ya ushirika na kilimo,wadau wa masoko na mitaji na sekta ya mifugo, lishe, chakula na mashine.
“Wengine ni pamoja na watoa teknolojia, ubunifu na uwekezaji, wadau wa madini, uvuvi na Saccos na wadau wote,” amesema.