Watakiwa kutumia 4R za Rais Samia

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amewataka wakulima na wafugaji wa Wilaya Kiteto mkoani Manyara kufanya maridhiano kwa kutumia 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ili kumaliza migogoro baina yao.

Makalla ameyasema hayo leo Septemba 9, alipozungumza na wananchi wa Engusero, wilayani humo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake katika mikoa ya Arusha na Manyara.

Amewataka wakulima na wafugaji wa eneo hilo kulindana na  kuheshimiana kwa sababu wanategemeana katika shughuli zao na kiuchumi.

Ameongeza kuwa wanapaswa kutumia 4R ili kufanya maridhiano kwani migogoro ya wakulima na wafugaji inaleta uhasama na inarudisha nyuma kiuchumi, hivyo wakiheshimiana wakakaa kwa amani watasonga mbele kibiasha na kiuchumi.

Habari Zifananazo

Back to top button