Watano wapoteza maisha Uturuki

UTURUKI : WATU  watano wameuawa katika shambulizi linalotajwa na serikali ya Uturuki kuwa ni la kigaidi kwenye Makao Makuu ya Kiwanda cha vifaa vya ndege cha Turkish Aerospace.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya amesema washambuliaji wawili walivamia kiwanda hicho, na kuwaua watu hao na kuwajeruhi wengine 22.

Taarifa  zinasema kuwa washambuliaji hao huenda ni wa Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi kilichopigwa marufuku nchini humo.

Advertisement

Kufuatia shambulizi hilo, vikosi vya anga vya Uturuki vimeamua kuharibu vituo 32 vya PKK vilivyopo Kaskazini mwa Iraq na Kaskazini mwa Syria.

SOMA: Uturuki kuipa Somalia ulinzi baharini