Watanzania wachangamkie fursa maeneo ya uwekezaji

SERIKALI imezindua maeneo matano ya kipaumbele kati ya maeneo zaidi ya 34 katika Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (SEZ) ambayo yametengwa kwa uwekezaji maalumu na ambayo yako tayari kwa matumizi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, maeneo hayo yana mchango mkubwa katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 (Dira 2050), ambayo inalenga Tanzania kufikia uchumi wa kati wa juu wenye pato la Dola za Marekani trilioni moja kwa mwaka ifikapo 2050.
Kwa mujibu wake, lazima uchumi wa nchi ukue kwa asilimia nane hadi 12 sekta ya viwanda imechaguliwa kuwa moja ya sekta kiongozi au sekta ya kimageuzi, hivyo imepewa kipaumbele kikubwa na serikali itaiangalia kipekee.
Maeneo matano ambayo yapo tayari kwa uwekezaji maalumu ni Kwala (Pwani), Nala (Dodoma), Buzwagi (Shinyanga), Bagamoyo Eco Maritime City (Pwani) na Benjamin William Mkapa (Dar es Salaam).
Katika kuvutia uwekezaji kwenye maeneo hayo, wawekezaji watapata huduma ya ulinzi, umeme, maji na barabara. Pia, mwekezaji atapata misamaha ya kikodi na serikali itatoa bure viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika maeneo hayo.
Tunaipongeza serikali kwa uamuzi huo wa kutenga maeneo hayo na kuwekeza vivutio kwa ajili ya wawekezaji wazawa kuweka humo na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi.
Hii ni hatua kubwa na ya kupongezwa kwa sababu inatoa unafuu kwa wawekezaji wazawa kukua kwani kwa kupewa unafuu, ina maana gharama za uwekezaji zitakuwa zenye kumsaidia mzawa kutekeleza miradi anayokusudia na hivyo kusaidiwa kukua.
Tunafahamu wapo wawekezaji wengi wazawa lakini wanashindwa kustawi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo mitaji midogo. Lakini vivutio hivi vinavyotolewa na serikali pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Mikopo ni uthibitisho mwingine wa Serikali ya Awamu ya Sita ilivyodhamiria kuwainua wawekezaji wazawa.
Kwa msingi huo, tunaamini wazawa watachangamkia fursa hizi kwa kuwa sehemu ya kushiriki katika mageuzi haya makubwa na hasa katika sekta ya viwanda na pia kuwa mstari wa mbele kuipeleka Tanzania katika nchi mpya ifikapo mwaka 2050, ambayo itakuwa miongoni mwa zile zenye uchumi imara duniani na inayojitegemea.
I not to mention my guys were looking through the good information on your web page and so all of the sudden came up with a horrible suspicion I had not expressed respect to the web site owner for those secrets. All of the men are actually totally excited to read them and already have truly been loving those things. Appreciation for really being really considerate as well as for getting variety of quality issues most people are really wanting to be informed on. Our honest apologies for not expressing gratitude to earlier.