Watatu wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Geita

GEITA; MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masijala ya Geita imewatia hatiani na kuwahukumu kunyongwa hadi kufa watuhumiwa watatu kati ya wanne wa Kkesi ya Mauaji Na. 29820 ya mwaka 2024 iliyoanza kusikilizwa Januari 07, 2025.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni Thereza Luhedeka (73) dada wa marehemu, Mateso Joseph (23) ambaye ni mtoto wa Thereza Luhedeka na Elias Galawa (49) ambaye ni mganga wa kienyeji.

Watuhumiwa hao wamepatikana na kosa la kushiriki kumuua Joyce Luhedeka (51), Mkazi wa Ikobe, Wilaya ya Mbogwe.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Oktoba 11, 2023 washtakiwa walimuua Joyce Luhedeka akiwa nyumbani kwake kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.

Imeelezwa baada ya washitakiwa hao kumuua Joyce Luhedeka, walizikata sehemu za siri na kutoweka nazo hadi walipokamatwa na kukutwa wakiwa wamezikausha.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button