Watatu wamekufa kula kasa

UFILIPINO : WATU watatu wamefariki na wengine 32 wamelazwa hospitalini nchini Ufilipino baada ya kula kasa wa baharini.
Maafisa wa usalama wamesema kuwa watu wengi kutoka jamii ya Teduray wameripotiwa kuharisha , kutapika na tumbo kuuma tangu kula kitoweo hicho wiki iliyopita katika mji wa pwani wa jimbo la Maguindanao del Norte.
Ingawa ni kinyume cha sheria kuwinda au kula kasa wa baharini chini ya sheria za ulinzi wa mazingira ya bahari nchini humo.
Lakini kasa wa baharini ambao hula mwani mchafu, wanaweza kuwa na sumu wanapopikwa na kuliwa.
Afisa wa eneo hilo Irene Dillo, aliiambia BBC, baadhi ya mbwa, paka na kuku waliolishwa kasa huyo pia walikufa.SOMA: Rais Samia azindua Utalii wa Kasa Kusini Unguja
tayari wameruhusiwa, huku watu watatu wameripotiwa kufariki dunia”, alisema Dillo.
Mwaka wa 2013, watu 68 katika Mkoa wa Samar Mashariki mwa Ufilipino waliugua na wanne kati yao walikufa baada ya kula kasa wa baharini.



