Watoto 500 kufanyiwa upasuaji JKCI

DAR ES SALAAM: Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto 500 katika kipindi cha mwaka mmoja yatakayogharimu Sh bilioni moja.

Fedha hizo zinatarajiwa kukusanywa Julai 6, 2024, kupitia chakula cha jioni (Dinner Gala) itakayofanyika jijini Dar es Salaam chini ya shirika lisilo la kiserikali la Heart Team Africa Foundation (HTAF) linaloshughulika na upatikanaji wa matibabu ya moyo kwa watoto wasio na uwezo.

Akizungumzia mpango huo leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dk Peter Kisenge amesema lengo la kutoa matibabu hayo ni kuokoa maisha ya watoto waliozaliwa na mgonjwa hayo kupitia HTAF na Tasisi hiyo.

“Takwimu zinaonesha kuwa watoto wengi wanazaliwa na matatizo ya moyo kati ya watoto milioni mbili wanaozaliwa kwa mwaka 14,000 wamakuwa na matatizo ya moyo na watoto 4,000 wanahitaji upasuaji”, amesema Dk Kisenge.

Dk Kisenge mbaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo amesema JKCI kwa mwaka uliopita  ilifanya upasuaji wa moyo kwa watoto 357 ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kufanya upasuaji kwa watoto 500.

Amesema kupitia Sh bilioni moja inayotarajiwa kukusanywa na HTAF, itawezesha kuwatibia watoto hao, hususan wale wa vijijini ambao hawana uwezo wa kugharamia huduma hizo.

Amesema, gharama za  matibabu ya moyo kwa watoto ni ghali hadi kufikia Sh milioni 10 kwa mgonjwa mmoja na Sh milioni 15 kwa upasuaji wa mtoto mmoja.

Akielezea kuhusu Dinner Gala hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo amesema kuwa katika usiku huo wa Dinner Gala, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete.

Habari Zifananazo

Back to top button