Watoto sita wenye vichwa vikubwa kulipiwa matibabu

DAR ES SALAAM: KIKUNDI cha Hisani cha Emma Kiduku Charity Group kimechangia matibabu ya watoto sita wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi wanaotibiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Ubongo Muhimbili (MOI).

Kiongozi wa kikundi hicho Emmanuel Madaha amesema lengo la kutoa msaada huo ni kusaidia kufanikisha matibabu ya watoto hao ambao wengi wao wanatokea kwenye familia duni na zisizojiweza kiuchumi.

“Tumekuja hapa kwa lengo la kusaidia watoto hawa wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa sababu wengi wao wanatoka familia zenye uchumi duni hivyo kushindwa kumudu gharama za matibabu yao” amesema. Emmanuel

Aidha, Emmanuel ameongeza kwa kusema kuwa licha ya kuchangia matibabu ya watoto hao lakini pia walitoa sabuni za maji lita 40 kwa ajili ya matumizi ya watoto hao.

Kwa upande wake, Ofisa Ustawi wa Jamii Msaidizi wa MOI, Yosephu Kuruba amesema MOI hupokea watoto wengi kutoka sehemu mbalimbali wakiwa hawana uwezo wa kuchangia gharama za matibabu, kupitia msaada huo utawasaidia watoto hao kufanikisha matibabu yao.

“Tunapokea watoto kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, wengi wao wakiwa hawana uwezo wa kugharamia matibabu. Hivyo msaada huu sio tu umeokoa maisha, bali umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi,” amesema  Yosephu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button